Thursday, 14 May 2009

Mwanahalisi Kumlipa Rostam Shilingi Bilioni Tatu!!!!


Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam jana iliamuru
wahariri pamoja na waandishi wa habari kumlipa Bwana
Rostam Aziz,mbunge wa Igunga kiasi cha shilingi
bilioni tatu(3bil.) ikiwa ni fidia kwa chombo hicho
cha habari kumdhalilisha bwana Rostam Azizi kwa
kuchapisha katika gazeti la Mwanahalisi habari isiyo
ya kweli na hivyo kumshushia heshima bwana Rostam Aziz.
Mwanahalisi ilichapisha habari iliyodai kwamba Rostam
Aziz ni fisadi na ni mtu mchafu katika jamii. Jaji
aliyesimamia kesi hiyo na kutoa maamuzi ni Jaji Robert
Makaramba ambaye alisema amefikia maamuzi hayo baada
ya gazeti la mwanahalisi kushindwa kutokea mahakamani kutoa ushahidi katika kutoa utetezi wake.Hata hivyo mwanasheria
wa gazeti la Mwanahalisi,Mtanzania Halisi bwana Marando
amesema kwamba tayari wameanza kuchukua hatua za awali kwa
ajili ya kukata rufaa.

No comments: