Saturday, 16 May 2009

Watazeeka kwa Umbea


Narudi zangu gheto kutoka kitaani nakuta masela zangu Imma na Nick rum wanagonga traki moja hivi ya Q-Chillah inaitwa 'itabidi wazoee'. . Nilipokaa baada ya muda hapo ndani nikashangaa kuona redio inapiga wimbo mmoja tu!! Nikawauliza jamani vipi mbona mmeweka "repeat"? Nick akajibu "mwana we acha tu hili songi la ukweli si kitoto". Na kisha akaniambia kuwa anazimika zaidi na mstari flani hivi kwenye huo wimbo.Mstari wenyewe unasema hivi "watazeeka kwa umbea ya kwetu yanatunyookea".Wimbo huu umetoka si siku nyingi na unaonekana kupendwa na wengi. Nasema hivyo kwa sababu baada ya muda mfupi akaja dada mmoja hivi wa chumba opposite na cha kwetu akasema "naomba muongeze sauti alafu msifunge mlango".Nayeye nilipomuuliza anapenda mstari gani katika wimbo huo akanijibu simpo tu kwamba "ndo ivo yani itabidi wazoee tu".Hongera Q-Chief kwa wimbo wako huu ambao unaonekana kuwashika wengi .Wewe je Mdau, unasemaje kuhusu wimbo huu? Tafadhali tupe maoni yako kwa kubonyeza hapo chini.

1 comment:

Anonymous said...

Wimbo bomba sana huo hata mimi naupenda sana.Ila sina uhakika kama umbea unazeesha.Mwenye jibu anipe.Malisa A.Malisa,A-Town.