Monday, 6 July 2009

BREAKING NEWS!!!

Habari zilizonifikia muda si mrefu zinasema kwamba raisi wa wanafunzi chuo kikuu Tumaini Iringa anafukuzwa chuo kutokana na pingamizi aliloweka baada ya kupanda kwa ada chuoni hapo.Chuo hicho kimeongeza ada kwa njia ya ujanja ujanja ambapo ongezeko hilo linatufanya wanafunzi tuushangae uongozi wa chuo.Baadhi ya mambo ambayo yanamfanya mzima yeyote na tena ambaye yuko timamu abaki mdomo wazi.Kwanza ongezeko limetangazwa wakati wanafunzi tunafanya mitihani,wakijua kwamba hatuna muda wa kuandamana na kufanya mgomo.Pili kufukuzwa kwa rais kunatokea baada ya wanafunzi kufunga chuo na kuondoka.Hii inatia mashaka sana kwa mtu mzima kama mimi.Mliopo Tumaini naomba mnithibitishie ukweli wa jambo hili.Asante kwa muda lakini badae kidogo ntaendelea kuleta habari zaidi kuhusu jambo hili.

No comments: