Friday, 8 May 2009

MANJI-"Sina Shida na Pesa za Mtu"


REGINALD MENGI

ROSTAM AZIZ

YUSUPH MANJI


Malumbano baina ya wanasiasa na wafanyabiashara kutokana na madai ya kudhalilishana yanavutia kimtindo ambapo mfanyabiashsra maarufu Yusuph Manji amefungua kesi dhidi ya bwana Mengi akidai kudhalilishwa na vyombo vya habari anavyovimiliki bwana Mengi. Hata hivyo kesi hiyo inaonekana kuvutia sana watu wengi hasa kutokana na madai ya bwana Manji kutaka alipwe shilingi moja tu(sh.1) pesa ya kitanzania."Shida yangu si pesa za mtu,ninachotaka kuona ni sheria inachukua mkondo wake na haki inatendeka".
Aidha wadau mbalimbali pamoja na wafatiliaji wa masuala ya siasa nchini wamedai kuwa hilo ni "DONGO" ama kashfa hasa kwa bwana Mengi ambaye "anajifanya kuwa ana pesa mingi" kufungua kesi zaidi ya kumi za madai ya kudhalilishwa huku akidai alipwe Bilioni moja katika kila kesi moja. Kwa mahesabu ya chapchap kama atawini kesi zote basi ana zaidi ya bilioni kumi.
"Mtu mwenye pesa kama huyu,atadaije pesa nyingi hivyo kutoka kwa waandishi na vyombo vya habari masikini?,Kwa nini asiige mfano wa "mtu mwenye pesa" Yusuph Manji ambaye kamdai Mengi shilingi moja tu?" alisikika mdau mmoja ambaye hakutaka jina lake lionekane katika blogu hii.Haya mpenzi msomaji na wewe una maoni gani kuhusu ishu hii?
Tupe maoni yako hapo chini.

No comments: