Thursday, 26 March 2009

Death Penalty,Adhabu ya Kifo,Wewe una Maoni Gani?

Kwanini Tanzania inasitasita kufuta adhabu ya kifo?Kifungu namba 14 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinasema kwamba “kila mtu ana haki ya kuishi”. Hii ni haki ya msingi ambayo kila mwanadamu anayo “kwa sababu tu kwamba yeye ni binadamu”.Haki hii haihitaji mtu kwenda mahakamani au katika vyombo mbalimbali vya haki na sheria ili kuipata, bali hupatikana kutokana na ‘kule kuzaliwa tu ukiwa binadamu’ kunakufanya uwe na haki hii ya msingi.Ndo sababu hata sheria ya Tanzania inakataza kuua kimakusudi,kutoa mimba pamoja na mambo mengine yanayofanana na hayo ya mauaji.
Kwa sasa duniani pote,nchi nyingi zinapigania kufuta adhabu ya kifo katika nchi zao ili kuendana na makubaliano ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo.Pia ili kutokwenda kinyume na katiba zao kwamba kila mtu ana haki ya kuishi.Hapa kwetu Tanzania adhabu hii bado inaendelea kufanyika licha ya Katiba yetu kujieleza waziwazi kwamba “kila mtu ana haki ya kuishi.Swali: Je,Serikali haioni vifungu hivyo katika katiba yetu hata ifumbe macho kiasi hiki? Mataifa mengine je kama Uganda,Rwanda.Burundi,Kenya n.k yanachukuliaje swala hili la adhabu ya kifo? Je, wewe una maoni gani kuhusu hili?

Nathamini sana mchango wako.Tafadhari sana usisite kutoa maoni yako hapo chini.
Ni mimi mwandishi wa Makala hii
Joram Frank
Tumaini University at Iringa
P.o.Box 200
Iringa,Tanzania.

1 comment:

Jo said...

Wadau msiogope kuchangia mada mbalimbali katika blogu hii.