Thursday, 30 April 2009

Mbunge Viti Maalum Ang'aka


Mheshimiwa Halima Mdee acharuka baada ya ripoti ya Bunge ya ukaguzi wa hesabu za serikali kuonesha kwamba kuna mchezo mchafu unaofanywa na viongozi wa serikari za mitaa pamoja na madiwani na mameya wa jiji.Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo,fedha hizo zimekuwa zikitafunwa vibaya mno.Badala ya kutumia fedha vizuri,pesa zimekuwa zikichotwa kwa kiasi kikubwa kisha kiasi kidogo kilichosalia kutumika katika mradi uliokusudiwa.Mheshimiwa alitoa mfano katika Wilaya ya Monduli ambapo Milioni 34 zilitolewa na serikali kwa ajili ya kujenga nyumba ya mwalimu lakini viongozi husika walitafuta mfadhili ambaye aliijenga nyumba hiyo kwa gharama zake mwenyewe.Haijulikani hadi sasa mamilioni hayo yamekwenda wapi.

Katika hali ya kushangaza,Mheshimiwa Mdee alitoa pia mfano wa hasara iliyosababishwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni baada ya kukataa ushauri wa madiwani na kufanya maamuzi yake binafsi hali iliyoisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 800.

Mchezo huu umekuwa ukifanyika kwa kasi sana ambapo ripoti za utekelezaji zinaonesha kwamba pesa zilizotolewa zimetumika ipasavyo lakini hali ni tofauti pale ambapo miradi tajwa ilitembelewa na wanakamati hao. Mfano ripoti moja ilisema kuwa bati 70 zimetumika kujenga choo lakini kamati ilipodai kuona choo hicho ilikuta ni bati 3 tu zilizotumika kujenga choo.Wizi Mtupu!!! Mchezo huu umekuwa maarufu sana hapa kwetu Bongo,serikali kuweni makini na mchezo huu.

1 comment:

Anonymous said...

Wizi mtupu!!!