Wednesday, 22 April 2009

Chid Benz na TID wazichapa laivu


Habari toka chanzo chetu zilidai kuwa, tukio hilo la aibu
lilitokea wiki iliyopita (Alhamisi usiku), ndani ya Club
Billicanas Posta, jijini Dar es Salaam, ambapo kulikuwa
na usiku wa kinadada ambao huruhusiwa kuingia bure huku
wanaume wakilipa kiasi kidogo taofauti na siku zingine.

Ilidaiwa kuwa, awali Chid akiwa na rafiki zake wawili
alitinga ukumbini hapo na kwenda kupozi karibu na DJ a
liyekuwa akisababisha vilivyo huku wakiwa na ‘monde’ (kinywaji)
mkononi.

Chanzo kilisema kuwa, haukupita muda mrefu ‘Top In Dar’
naye alitinga ukumbini humo akiwa na kundi lake wakiwa
‘fulu kinywaji’, ambapo moja kwa moja walikwenda kunakouzwa
‘moja baridi, moja moto’ (kaunta) na kuketi.

Huku akizungukwa na warembo waliokuwa wakimtaka akacheze
nao muziki, TID alishutushwa na kundi lililoongozwa na Chid,
lililovamia warembo wale, kisha kumtishia kumshushia kichapo
mkali huyo maarufu kama sauti ya gerezani.
Chanzo kiliendelea kusema kuwa, TID hakuwa tayari kukutwa na
fedheha hiyo mbele ya ‘totozi’ hivyo alilazika kuonesha maujuzi
ya kurusha ngumu aliyolambishwa toka gerezani.

Ilisemekana kwamba, Chid kama kiongozi wa kundi lake, naye
alijikuta akionesha ubabe wa ‘kitaa’ pale alipomrukia TID na
kujikuta wakizichapa kavukavu.

Baada ya vurugu hilo ambalo lilikuwa ni soo tupu, mabaunsa wa
ndani ya kiwanja hicho walilazimika kuingilia kati kuamulia ngumi
hizo zilizokuwa zikirushwa na mastaa hao kama mvua ya mawe.
Katika timbwili hilo, TID alisikika akidai kuwa, haogopi jela, hivyo
alitaka kumuonesha Chid ‘mbivu na mbichi’ siku hiyo hadi aite maji ‘mma’.

Hata hivyo, kiongozi wa mabaunsa hao (jina tunalo) aliamuru TID
na Chid watolewe nje ya ukumbi huo, kisha kufungiwa kabisa kutinga
katika kiwanja hicho cha maraha.

No comments: